English Spanish

Taswira ya kunyang’anywa ardhi: kutathmini upangwaji upya wa hifadhi inayoongozwa na serikali, Saadani, Tanzania

Alejandra Orozco-Quintero and Leslie King
Ilichapishwa katika Journal of Political Ecology 2018. 25: 40-63.

Nadharia

Maeneo yanayohifadhiwa yanatajwa kama “simulizi ya mafanikio muhimu zaidi ya uhifadhi”, yamekuwa ni njia inayopendelewa zaidi na miongoni mwa wakuu wa kitaifa katika maafikiano ya Biolojia anuai ya kuelezea changamoto zinazokabili uhifadhi wa mazingira. Hata hivyo maeneo ya hifadhi yaliyo chini ya mamlaka za kiserekali zimekuwa zikikosolewa kwa kushindwa kufikia malengo ya kiikolojia na kijamiii ya kuanzishwa kwao. Kufikia maakubaliano juu ya mikakati ya uhifadhi wa wanyamapori, hayajaweza kuelezea meneo ya hifadhi ya serekali kukubaliwa na jamii. Mijadala inahoji kama serikali ina nia ya dhati na ufanisi inapofaya kazi yake ya udhibiti. Makala hii inatoa tathmini ya uhifadhi unaosimamiwa na serikali katika eneo la Saadani, nchni Tanzania, ukiangalia njia iliyofuatwa katika kuanzisha maeneo ya hifadhi. Kuanzishwa kwa shughuli za uhifadhi zimepelekea watu waliojitolea kushiriki katika uanzishaji wake kutolewa katika maeneo yao.

Hii imekuwa ni kinyume na sera za uhifadhi za Tanzania zinazoelezea njia shirikishi. Kupitia njia iliyotumiwa naserikali kuanzisha shughuli za uhifadhi Saadani, tutaelezea namna ambavyo njia iliyotumiwa na serikali imekuwa na manufaa kufikilia maazimio ya serikali na kuleta madhara kwa wanajamii wanaosaidia uhifadhi.  Kwa kuzingatia mtazamo wa mashirika yanayosaidia uhifadhi Tanzania, makala hii inapendekeza kupitiwa upya kwa sera za uhifadhi duniani na kuainisha njia za kutunza haki za mipaka na makazi ya jadi katika mameneo yanayokusudiwa kwa uhifadhi.

Utangulizi 

Karne moja baada ya kuanzishwa kwake, modeli ya Hifadhi ya Taifa ya Yellowstone, inayojulikana pia kama “fortress conservation”, imekuwa ni kivutio kikubwa cha uhifadhi wa mazingira asilia duniani (Brockington 2002).

Ilitambulika rasmi kama eneo linalohofadhiwa mwaka 1991 likiwa na wanyama wasiozidi elfu saba (7000) na kufikia 209,000 mwaka 2014 (Juffe-Bignoli et al. 2014).

Hata hivyo, kuna kauli ya kushtua iliyotolewa mwaka 2010 baada ya kutambulika kimataifa kuwa, licha ya ongezeko la wanyama na kupanuka kwa eneo la hifadhi hiyo, imeshindwa kufikia malengo yaliyowekwa na serikali za dunia mwaka 2002 ya kupunguza upotevu wa bayoanuai duniani kwa ngazi za kimkoa na kitaifa kama mchango wa kupunguza umasikini na kwa manufaa ya maisha aina zote duaniani. (Secretariat of the Convention on Biological Diversity 2010: 9).

Kufuatia hili, mwaka 2010, vyama 192 vya majimbo vilivyohudhuria Convention on Biological Diversity (CBD) vilibadilisha malengo yao ya kimazigira kwa kuafikiana kuweka jitihada zaidi kuzuia ongezeko la upotevu wa bayoanuai duniani (Juffe-Bignoli et al. 2014). Malengo hayo yaliyohifadhiwa katika Aichi Biodiversity Targets (Malengo ya Bayoanuai ya Aichi) yaliyoafikiwa na kongamano la vyama hivyo mwaka 2010, Nagoya, ni pamoja na kuhifadhi 17% ya maeneo ya maji yaliyo ndani ya maeneo ya nchi kavu, na 10% ya mwambao na bahari kuwa chini ya hifadhi ifikapo 2020 (Convention on Biological Diversity 2010).

Mwaka 2014 taarifa ya UNEP’s Protected planet (Dunia iliyohifadhiwa) iliainisha 15.4% ya uso wa dunia kuwa ni Maeneo yanayohifadhiwa (Juffe-Bignoli et al. 2014). Mfumo unaotumiwa kimataifa wa malengo ya kukuza maeneo yanayohifadhiwa (PAs) unajumuisha malengo mengi tofauti na ya aina tofauti za usimamizi (usimamizi wa serekali, wakazi asilia, sekta binafsi, na ushirika mchanganyiko) (IUCN 2009). Lakini kufikia mwaka 2014 miongoni mwa maeneo yote yanayohifadhiwa (PAs) yatoayo taarifa kwenye kumbukumbu za duania ya Maeneo yanayohifadhiwa (World Database of Protected Areas -WDPA), kwa kiasi kikubwa zilifuata modeli ya maafikiano (conventional model). Taarifa ya UNEP ilionesha kuwa 88% yalikuwa yanasimamiwa na serikali ambapo 1% pekee ilikuwa inasimamiwa na wakazi asilia na jamii (Juffe-Bignoli et al. 2014), na 64% ya maeneo yote yanayohifadhiwa ( PAs) yenye malengo yaliyoorodheshwa, angalo nusu yake yalikuwa katika kundi la (maeneo ya) vizuizi. Miongoni mwa haya maeneo yaliyo katika vizuizi, 26.6% yanawekwa katika kundi la Hifadhi za Taifa (Juffe-Bignoli et al. 2014).

Ingawa takwimu juu ya idadi ya Maeneo yanayohifadhiwa (PAs) chini ya kila kundi la IUCN inaonesha kuwa hifadhi za taifa zipo katika kundi dogo, yanachukua maeneo makubwa zaidi na hivyo kufanya kuwa njia inayotumiwa zaidi katika uhifadhi wa baoanuai. (Chape et al. 2008). Kwa kuwa uhifadhi wa kisasa unategemea zaidi modeli hii kuna haja ya kuelewa vema faida na mapungufu yake, na kuchukua hatua za kuboresha au kufanya mabadiliko.

Wakati upotevu wa bayoanuai ni matokeo ya vitu vingi, ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, viwanda na upanuzi wa shughuli za kilimo, na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali, machapisho ya taarifa zote mbili za CBD 2010 na UNEP 2014 zinathibitisha umuhimu wa Maeneo yanayohifadhiwa (PAs). Kuna vithibitisho mkubwa kuwa Uhifadhi wa kutenga (jamii) una madhara makubwa kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo yanayohifadhiwa ambazo zinazotegemea ardhi yenye bayoanuai. Miongoni mwa (vithibitisho) hivi ni Tathmini ya Chase (1987) juu ya madhara hasi ya sera zinazoundwa juu hususan wadau wa uhifadhi waliokosa kuunganika wa Hifadhi ya Yellowstone, pamoja na mapitio ya kukosekana kwa mfumo sahihi na madhara ya kutumia modeli ya “Hifadhi ya kijeshi” kwenye maeneo yaliyokua na muingiliano wa watu na mazingira asilia (Brockington et al. 2008; Chapin 2004; Dowie 2011; West and Brechin 1991; West et al. 2006).

Katika hali ya kuongezeka kwa jitihada za serikali na malengo ya dunia ya kuongeza maeneo yanayohifadhiwa (PAs) (Juffe-Bignoli et al. 2014; Venter et al. 2014), kuna maswali muhimu yanayohitaji kuangaliwa. Je, migogoro iliyopo ya kitaasisi kwenye maeneo ya hifadhi yanayosimamiwa na serikali hutokana na utofauti wa modeli shirikishi na ambazo si shirikishi kwa usimamizi wa mazingira asilia au inaashiria kitu kingine? Kwa namna gani usimamizi shirikishi wa maeneo ya hifadhi yanayosimamiwa na serikali unaweza kuathiri ufanisi wa uhifadhi au uendelevu wa kijamii wa maeneo yanayohifadhiwa (PAs)? Kwenye nchi rafiki kwa uhifadhi kama Tanzania, ambapo theluthi moja ya eneo lake linawekwa katika kundi la maeneo yanayohifadhiwa (PAs)  (IUCN and UNEP 2013), na uhifadhi umekuwa ukipendelewa na kupigiwa debe na taasisi za serikali tangu wakati wa ukoloni(Goldstein 2004),utungwaji wa kanuni wa kutoka ngazi za juu umesababisha migogoro kati ya jamii na taasisi za serikali na wameshindwa kufikisha matunda ya uhifadhi kwa jamii zinazoathiriwa au zinazopakana na hifadhi za Taifa (Brockington et al. 2006; Goldman 2003; Neumann 1998).

Kwa hali hii, lengo kuu la makala hii ni kuangalia kwa kina njia ya uanzishwaji wa maeneo yanayohifadhiwa na athari ya njia za uhifadhi zinazotumika. Inaongezea uzito kwa vithibitisho ambavyo tayari vipo juu ya kutoendana kati ya utengenezwaji kanuni unaofanywa na ngazi za juu na mifumo ya uhifadhi ya kijamii katika kutekeleza uhifadhi wa bayoanuai.

Hata hivyo, malengo yake makuu ni zaidi ya kuandika juu ya athari za uhifadhi unaosimamiwa na serikali wa “uhifadhi wa kijeshi”, kuelezea baadhi ya njia zinazotumiwa na serikali katika usimamizi. Inaelezea njia za uanzishaji unaofanywa na taasisi zilizowekwa kimataifa, ambazo mara nyingi hupuuzwa, zinazosimamia utekezaji wa uhifadhi na namna ambavyo zinapuuza nafasi za taasisi mbalimbali katika uhifadhi wa bayoanuai na zimekuwa kikwazo kufikia malengo ya muundo wa uhifadhi wa dunia.

Usimamizi wa maswala ya Uhifadhi 

Maeneo yenye utajiri wa kibayoanuwai na kitamaduni hutofautiana na huleta muingiliano mwingi kati ya binadamu na viumbe hai asilia (Zimmerer and Young 1998). Kuanzishwa kwa maeneo haya kunaathiri na kuathiriwa na huu muingiliano, zinaelezewa katika muundo ambao makazi, uhifadhi na kupata maisha kunaunganishwa kwa maeneo yaliyotengwa (Berkes, Folke and Colding 1998; Roth 2008), na matumizi anuai na kuishi kwa kutegemeana (Colchester 1994).

Leo, idadi kubwa ya tafiti, ikiwa ni pamoja na tafiti zinazojumuisha hifadhi namaeneo ya hifadhi ya jamii zinatoa mifano mizuri ya kuanzishwa na ushirikishwaji wa jamii katika kusimamia mazingira asilia. Utofauti huu umekuwa ukifafanuliwa kwa namna tofauti na wahusika wa uhifadhi kwa ngazi tofauti katika jamii (Roth 2008; Zimmerman 1995).

Mtazamo wa bayoanuai na njia zinazotumika kuhifadhi zinawekwa sawa na michakato ya kimila na kisiasa na mahusiano (kati ya taasisi, jamii na mazingira). Njia za uhifadhi zenye misingi ya kisiasa, zinatumika kusemea mahusiano hayo rasmi na matokeo yake. Taasisi ni vipengele muhimu vya serikali vinavyotengeneza vifungu vya kanuni, haki na michakato inayokusanya maamuzi na utendaji, huwa na mchanganyiko wa wahusika na kuongoza mchangamano wao (Young 1999). Taasisi katika kila ngazi ya kijamii zipo katika mvutano muda wote na zinawajibika na taasisi nyingine za ngazi za juu au ngazi za chini zaidi (Underdal 2008). 

Katika hali isiyoridhisha, umiliki wa ardhi kimila na kwa ngazi za chini mara nyingi umekuwa ukivurugwa na taasisi za hifadhi za serekali. Katika uhifadhi wenye sheria kali unaosimamiwa na serekali, usimamizi wa maeneo yanayohifadhiwa hutumika kama njia ya kupunguza uharibifu unaosababishwa na binadamu kwa kuondoa jamii za watu, kwa vile hii inadhaniwa italeta matokeo mazuri katika kuhifadhi wa bayoanuai.

Hata hivyo njia hii ya uhifadhi imekuwa ikihojiwa kutokana na madhara inayosababisha kwa jamii ambazo ardhi yao imekuwa kwa muda mrefu imemea bayoanuai asilia na pia kwa wanyamapori ambao maeneo ya hifadhi yanakusudiwa kuwatunza. (Benjaminsen et al. 2013; Benjaminsen and Bryceson 2012; Brechin, Murray et al. 2007; Brockington 1999; Chapin 2004; Dowie 2011). Hakika, matokeo mazuri katika uhifadhi ni kitu ambacho hakijazoeleka kwenye maeneo yanayohifadhiwa (Craigie et al. 2010; Mora and Sale 2011; Packer et al. 2011).

Mafanikio yasiyowiana katika uhifadhi yanaweza kusababishwa na vitu vingi, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, hali ya kiikolojia na uchumi wa jamii (Venter et al. 2014; Watson et al. 2014; Wilson 2002). (Barrett et al. 2001; Brandon et al. 1998), kadhalika njia ambazo uhifadhi unafanyika unaashiria namna soko linavyoondeshwa (Igoe and Brockington 2007; Peterson and Isenhour 2014). Hii ni mienendo ambyo imewekwa kutokana na uchambuzi wa sera na usimamizi Tanzania (Brockington et al. 2006; Benjaminsen and Bryceson 2012; Benjaminsen et al. 2013; Neumann 1998), na duniani (Chapin 2004; Dowie 2011).

Hususan, maendeleo ya uhifadhi unaosimamiwa na serekali unaochechemea kwa zaidi ya karne umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kufikia malengo ya jumla ya kijamii na kiikolojia.  (Aubertin and Rodary 2011; Benjaminsen and Bryceson 2012; Brandon et al.1998; Barrett et al. 2001; Brockington et al. 2008; 2011; West and Brechin 1991). Zaidi, mfumo wa serekali wa uhifadhi wa Maeneo yanayofadhiwa (PAs) inabaki kama alama ya jitihada za uhifadhi (Juffe-Bignoli et al. 2014), na ndio zilizosambaa zaidi na kufadhiliwa kwa kiasi kikubwa (James et al. 1999; Waldron et al. 2013).

Muundo wa sasa wa dunia unaosimamia jinsi nchi zinavyoelezea uhifadhi wa bayoanuai unajumuisha si tu malengo yanayogusa pande zote ya uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi, bali pia malengo ya ngazi tofauti yaoAichi. Kwenye mkutani wa kumi wa kongamano la vyama vya uhifadhi wa bayoanuai wa mwaka 2010, mpango uliopitiwa upya ulitumika na katika muhimili wake ulikuwepo mpango wa malengo wa Aichi wa 2011-2020. Hizo ndio hatua serekali zilikubaliana kutumia kuboresha mipango kazi ya taifa inayoundwa.

Malengo ya tano ya viumbe hai ya Aichi

 

  1.  Kuainisha sababu za msingi za upotevu wa bayoanuai kupitia kwa kuingiza masuala ya viumbe hai kupitia serekali na jamii;
  2.  Kupungza matumizi makubwa ya bayoanuai na kukuza matumizi endelevu;
  3.  kuboresha hali za bayoanuai kwa kulinda utofauti wa mazingira, na aina za viumbehai.
  4.  kuwezesha mafanikio kwa wote kutokana na huduma za bayoanuai na mazingira na;
  5.  kuwezesha utekelezaji kupitia mipango shirikishi, upeanaji wa taarifa na uwezeseshaji.

Bado haijaelezwa ni kwa kiasi gani mallengo haya matano yamefanyiwa kazi na kubadilisha ufanyajikazi wa serekali. Mpango wa uhifadhi unalenga (17% ya nchi kavu na 10% mwambao nabahari zihifadhiwe), licha ya kuwa mashuhuri ni miongoni mwa malengo haya matano. Hadi sasa, tafiti zinaonesha changamoto katika ngazi za utengenezaji mipango na usimamizi, na haja ya kutambua madhara yanayosababishwa na njia zinazotumika kuendesha uhifadhi. Mbali ya maswali juu ya vipengele vya upangaji na usimamizi, kuna swali juu ya nini kifanyike, changamoto hizi pia zinahimiza utafiti ili kujibu maswali ya nani na namna ya kufanya maamuzi, pamoja na uchambuzi wa kina wa miundo inayoongoza utengenezaji na utekelezaji (Robinson and Makupa 2015; World Resources Institute et al. 2003).

Kwa miaka thelthini iliyopita, kumekuwa na maendeleo kuelekea uhifadhi shirikishi (Borrini-Feyerabend et al. 2004; Brechin, Wilshusen et al. 2003). Pia kumekuwa na ongezeko katika uelewa wa namna gani mitazamo inavyoweza kusababisha migogoro na fursa kati ya wanajamii na idara za hifadhi (Roth 2008). Hata hivyo, licha ya kutambua madhara ya utungaji wa mikakati unaofanywa na ngazi za juu, (Rantala and Vihemäki 2011), ya kuondosha watu katika maeneo ya jadi kwa kisingizio cha uhifadhi (Brockington and Igoe 2006; Dowie 2011) na katika kutambua tofauti kati ya uhifadhi unaowawezesha jamii na ule unaowatenga jamii (Alcorn 1993; Borrini-Feyerabend et al. 2004; Colchester 1994; Stevens 1997),

utafiti bado haujagusa mipaka ya hifadhi inayosimamiwa na serekali na uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi (PAs), inayodhaniwa kuwa inaweza kufanyika vema kwa mchakato shirikishi. Makala hii inaangalia mchakato na njia inayotumiwa na serekali ya Tanzania katika uanzishwaji wa hifadhi ya Taifa ya Saadani na njia za uhifadhi wake. Inaelezea jinsi serikali ilivyofanya maamuzi, kuweka mipango na kutengeneza mipaka ya Hifadhi, Saadani – ambayo mwanzo ilikuwa pori la akiba na baadae kuwa hifadhi ya Taifa – na namna gani hili limesababisha kukandamiza maisha ya watu na kupoteza haki za kibinaadamu.  Tunarai kuwa uhifadhi unaosimamiwa na serekali unaotumia kanuni za zamani za kusimamia uhifadhi kwa kutenga jamii, inaweza kuchangia kukwamisha malengo ya duania ya uhifadhi wa bayoanuai. 

Hifadhi ya Taifa ya Saadani

Hifadhi ya Taifa ya Saadani (SANAPA), ilianzishwa mwaka 2005, na nihifadhi yenye umihimu mkubwa miongoni mwa Hifadhi za Tanzania kwa sababu ya mazingira yake ya kibaolojia, kiikolojia na kijamii, pamoja na sehemu iliyopo katika Pwani ya bahari ya Hindi. Ni hifadhi ya kwanza kwa ndani ya nchi inayojumuisha shehemu ya bahari nan chi kavu (kama inavyooneshwa kwenye picha na. 1). Hifadhi ipo katika wilaya za Pangani, Handeni (Mkoa wa Tanga) na Bagamoyo (Mkoa wa Pwani). Hifadhi imezungukwa na vijiji kumi na saba (17) vinavyotambulika rasmi na venye serekali zinazofanya kazi. Vijij hivi vinajumuisha vijiji kumi na vitatu (13) ambapo viliguswa na tafiti huu: Saadani, Buyuni, Mkwaja, Mikocheni, Mkange, Kwakibuyu, Gendagenda, Mbulizaga, Mkalamo, Kwamsisi, Mkange, Gongo and Matipwili. Vijiji vinavyopakana vina muunganiko wa kiasili na hifadhi hili kwa shughuli za kimila, makazi na namna ya kupata maisha yao.

Picha 1: Hifadhi ya Taifa ya Saadani na vijiji vya karibu ambavyo vilihusishwa katika utafiti huo. Chanzo cha Chanzo: Mpango wa Usimamizi wa Hifadhi ya Saadani, mipango ya matumizi ya ardhi ya kijiji na data za msingi za eneo. Hifadhi ya Kwanza katika nchi inayojumuisha maeneo ya baharini na duniani.

   

Sera ya Hifadhi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa juu ya uanzishwaji wa hifadhi na usimamizi

Juhudi za awali za majaribio za TANAPA za kuifikia jamii zilianza mwaka 1988, na imekuwa katika mpango wao wa Taifa wa ujirani mwema: Community Conservation Services (CCS) (Tanzania National Parks Authority 2005). CCS imekuwa ni muundo rasmi ndani ya TANAPA mwaka 1992, na kwa sasa ni kitengo kamili chenye watumishi wa kudumu katika kila hifadhi ya Taifa. Mpangokazi wa kitengo cha CCS: 2005-2015 umekusudia kuongeza uhusiano na ushirikiano na jamii na wadau mbalimbali ili kufanikisha malengo makuu ya TANAPA.

Hata hivyo, kama ilivyowekwa, mpango shirikishi umetajwa mara moja tu ndani ya kitabu cha sera cha sera kama moja ya misngi ya TANAPA. Kwa nyongeza, jitihada za TANAPA katika usimamizi shirikishi zinaelekezwa zaidi kwa jamii zinazopakana na hifadhi, si zile zilizopo ndani. Malengo makuu ya mpangokazi huo ni kufanikisha kati ya asilimia 50% na 80% ushirikishwaji wa jamii zilizopo pembezoni mwa hifadhi kunufaika pamoja na shughuli za usimamizi wa maliasili, asilimia 25% ya hizi jamii zina mipango ya matumizi bora ya Ardhi. Kwa kuongezea, mpangokazi unajumuisha misaada kwa miradi ya kuiwezesha kijamii, mafunzo na kujenga uwezo kwa watumishi na jamii ili kukuza uhusiano wa kitaasisi na kupunguza ujangili na miigogoro baina ya jamii na hifadhi.

Sera hizi zitapewa nguvu na jitihada zingine, ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa ngazi mbalimbali, kujenga uwiano kati ya matumizi ya rasilimali na sharia za uhifadhi na miundo ya kisheria ya ngazi za juu na ngazi za chini – programu za utafiti; na kukuza vyanzo mbadala vya mapato na michakato mingine inayoanzishwa na hifadhi (Tanzania National Parks Authority 2005).

Kwa muongozo wa TANAPA, Sera ya hifadhi ya Taifa ya Saadani ya usimamizi shirikishi ina vipengele vine vya kufanyiwa kazi (Tanzania National Parks Authority 2009): 

  1. Program ya utunzaji wa mazingira; 
  2. Program a usimamizi wa utalii;
  3. Program ya ujirani mwema;
  4. Program ya kazi za hhifadhi.

Kama inavyoelezwa kwenye mpango, program ya Ujirani mwema imekusudiwa kuleta uwezeshaji wa jamii na ushirikiano, kutunza sifa ya hifadhi kwa kuongeza elimu ya uhifadhi na mawasiliano na ushirikiano kati ya hifadhi na jamii (Tanzania National Parks Authority 2009:  5).

Njia zilizotumika katika utafiti na ukusanyaji wa data

Mradi mkuu wa utafiti huu umechukua kipindi cha ya miezi 18 kuanzia mwaka 2012 hadi 2014 katika vijiji 13, (picha na.1), kuzungumza na viongozi wa jamii, viongozi wa serekali za vijiji, wasimamizi wa hifadhi, na mamlaka za serekali kwennye hifadhi za bahari, ardhi, na mipango ya matumizi ya rasilimali kwa ngazi za wilaya na mkoa. Mahojiano yalifanyika na watu 217 kwa makundi maalum. Makala hii inaegemea matokeo ya utafiti kuhusiana na mahusiano ya uhifadhi na matokeo yake kati ya hifadhi ya Taifa ya Saadani na Jamii. Kwa kuongezea, machapisho mbalimbaili yalikusanywa kutoka ofisi za serekali, vijiji na vyanzo binafsi (vilivyowekwa katika machapisho na ambavyo havijawekwa katika machapisho), yanayohusiana na uanzishwaji wa Hifadhi, kanda za usimamizi, matumizi ya ardhi ya vijiji na mipangilio ya rasilimali na data nyenginezo.

Walioshiriki katika utafiti ni pamoja na viongozi wa vijiji na wazee katika taasisi na serekali za vijiji. Watoa taarifa wa msingi ni pamoja na mamlaka za wilaya na mkoa na watumishi wa serekali kutoka Tanga, Dar es Salaam na wilaya za Handeni, Pangani na Bagamoyo. Waliohojiwa mmoja mmoja ni pamoja na wahifadhi wanaohusika na ulinzi wa rasilimali, ujirani mwema na ikolojia na watumishi wa utawala wa hifadhi. Uchambuzi wa taarifa umefanywa kwa kutumia program ya NVivo. Ukusanyaji wa data ulijumuisha uchukuaji wa nukta za GPS na mipaka ya hifadhi ya alama za mawe (bikoni), mipaka ya jamiii na eneo linalohifadhiwa, vituo vya vijiji na maeneo mengine yanayohusika na maeneo yenye migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na vijiji.

Pia kulikuwa na kutembea msituni na sehemu zingine kukusanya taarifa pamoja na viongozi wa vijiji na watu wengine muhimu katika utoaji wa taarifa. Kwa ujumla wake, taarifa zilizokusanywa zilijumuisha nukta za GPS na taarifa zaidi kutoka katika mipango ya matumzi bora ya ardhi za vijiji, mipaka ya hifadhi, maeneo ya hifadhi ya vijiji na taarifa zingine za makazi ya vijiji na maeneo maalumu. Uchambuzi wa taarifa ulitumia program ya ArcGIS ili kutoa ramani za kidigitali na vifaa vingine vya kuonesha maeneo ya kijiografia, kutegeza ramani na kufanya uchambuzi wa kutumia picha. Hii ilijumuisha kuainisha mipaka ya asili kwa kutumia taarifa zilikusanywa kwa kifaa cha GPS na ramani za kidijitali, kutengeza ramani zaidi kuonesha maeneo maalumu na utofauti wa mipaka, kuelezea njia zilizotumika katika eneo la Saadani.

Matokeo ya Utafiti  

 Kuingiliwa kwa ardhi kabla ya kufika Hifadhi ya Taifa ya Saadani

Kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilikuwa ni moja ya vamizi kadhaa za ardhi la eneo la Saadani. Uvamizi wa kimaendeleo wa mwanzo katika eneo la Saadani ulikuwa ni miaka ya 1950 ilipoanzishwa ranchi ya Mkwaja (Pangani District Archives). Picha na. 2, imepatikana kutoka kumbukumbu za wilaya ya Pangani, inaonesha mipaka ya mwanzo ya ranchi. Kama inavyoweza kuonekana baadae kwenye picha na. 6, ranchi ya Mkwaja ilichukua zaidi eneo la kaskazini la Hifadhi ya sasa ya Saadani. Viongozi wa vijiji 13 vinavyopakana na hifadhi wanaona ranchi ya Mkwaja ilikuwa na athari katika kuendelea kwao kiuchumi kwa kipindi cha miaka minne (4) iliyodumu ranchi hiyo.

Picha 2: Ramani ya awali ya historia ya Mkwaja Ranch ya zamani. (Chanzo: Archives za Wilaya za Pangani) .

Njia zngine mbili za kuingiliwa kwa ardhi ya eneo la Saadani ilikuwa ni kuanzishwa kwa Pori la akiba la Saadani (Saadani Game Reserve (SGR)), lililoanzishwa rasmi mwaka 1974 (lakini lilianza kufanya kazi tangu 1968) (Department of Wildlife and The Republic of Tanzania 1968) na pori la akiba la Zaraninge lilipendekezwa mwaka 1990s na kuanzishwa rasmi mwaka 2000 (Tanzania National Parks Authority 2003). Kiwango cha uelewa wa vijiji vya Saadani juu ya uhifadhi wa mazingira ulichangiwa na kuanzishwa pori la akiba la Saadani (Mwinyamane 1994, 2003). Utafiti unaonesha kuwa Pori la akiba la Saadani lilikuwa ni matokeo ya jitihada za viongozi na wazee wa kijiji na viongozi wa idara ya wanyamapori kuwezesha hifadhi na makazi ya watu kuwepo kwenye eneo moja.

Wakiwa wanashiriki kazi ya jumuiya miaka ya 1960, wanakijiji wa Saadani walimuona aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori, Bw. H.S. Mahinda, aliyekuwa akipita kijijini kuelekea Pangani. Wakiwa na nia, wanakijiji waliomba msaada wa Bw. Mahinda kusitisha wanyama kuuliwa kulikokuwa kukifanywa na watu kutoka nje na wilaya za pembeni (Mwinyamane 1994, 2003). Mazungumzo haya yalipelekea kuanzishwa lililokuja kujulikana kama Pori la Akiba la Saadani lilioanzishwa na kusaidiwa na wanakijiji mwishoni mwa miaka ya 1960s (Mwinyamane 1994, 2003).

Vielelezo vinavyoonesha mchakato wa uanzishwaji, makubaliano na kuonesha mipaka halisi ya eneo la pori la akiba havikupatikana katika maktaba ya Taifa ya Tanzania. Hata hivyo, kumbukumbu zingine ikiwa ni pamoja taarifa za mwaka – baadhi zimeandikwa kwa mkono na kusainiwa na Bw. Mahinda za mwaka 1968 – zinaonesha sera za kitengo cha wanyamapori kuelezea uhifadhi kwenda bega kwa bega na jamii. Taarifa hizi zinaelezea jitihada za kuwezesha jamii kushiriki kusimamia utalii na ufanyaji maamuzi shirikshi (Department of Wildlife and The Republic of Tanzania 1968). Taarifa kutoka kwenye mahojiao na wazee pamoja na taarifa za kihistoria za SGR na vielelezo kutoka kijijini vinaonesha kuwa SGR iliruhusu ushirika wa ngazi tofauti, kujenga kuaminiana, ufanyaji maamuzi shirikishi, usimamizi wa pamoja wa wanyamapori na kukua kwa uhifadhi wa kiikolojia katika miongo mitatu ya kuwepo kwake.

Katika mpangilio wake, taarifa za SGR hazioneshi kuwepo mapendekezo ya kuvionndoa au kuvihamisha vijiji vya Pwani isipokuwa maeneo mawili ya vitongoji ambavyo viliondoshwa kwa sababu vilikuwa katikati ya eneo lililopendekezwa la pori la akiba (mojawapo kilijulikana kama Tengwe) (Department of Wildlife and The Republic of Tanzania 1968). Picha na. 3, imetolewa kutoka taarifa ya kiufundi ya mwaka 1997 kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, inaonesha sehemu zote tatu zilizoingiliwa: Mkwaja Ranchi, SGR na Msitu wa akiba wa Zaraninge). SGR imeoneshwa kama na. 3, kaskazini mwa eneo lenye Ranchi ya Mkwaja, na Msitu wa Zaraninge umeoneshwa magharibi mwa SGR na imeonesha kama na. 4 kwenye ramani. Pia katika ramani ya ripoti ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, SGR imeoneshwa kijiografia (Picha na. 4).

Kielelezo cha 3: Ramani ya kale zaidi ya Hifadhi ya Saadani ya Hifadhi ilipatikana hadi sasa. (Chanzo: Ripoti ya Utafiti wa 1997 iliyotumiwa na Idara ya Wanyamapori kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Maktaba ya IRA: Ref No. T4 196.6.T34 E68).

Matoleo yote mawili ya ramani za SGR zinaeleza kuwa sehemu ndogo ya pwani iliingizwa kwenye eneo la hifadhi ya akiba. Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa ufukwe wa hifadhi ya akiba “si mpana kama ambavyo inadhaniwa”. Kwa uhalisia, “ni hadi kilometa 2.5 ya ufukwe kutoka Mto Mvave”, eneo kubwa la ufukwe lipo katika kitongoji cha Uvinje kilichopo kaskazini mwa kijiji cha Saadani hadi Mdomo wa Kijitokombe, kwa upande wa kusini eneo hili limechukuwa ufukwe wote wa hifadhi ya akiba (University of Dar Es Salaam and Institute of Resource Assessment 1997: 3).

Kielelezo cha 4: Toleo la kijiografia la SGR linalotokana na ramani ya kale kabisa (Mchoro 3) pia imepatikana katika ripoti ya 1997 kuhusu utafiti uliofanywa na Idara ya Wanyamapori kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Ref No. T4 194.6.T34 E68 ).

Yaliyomo katika taarifa hiyo ya Chuo kikuu cha Dar es salaam ni muhimu kuthibitisha mpangilio ulivyokuwa wakati wa uanzishwaji wa hifadhi, kwa kuwa taarifa ilisimamiwa na Idara ya Wanyamapori yenyewe, na inaendana na mipaka ya eneo la pori. Mipaka ya mwanzo ya SGR ya mwaka 1974 ni muhimu katika kuelewa maafikiano kati ya Idara ya wanyamapori na kijiji cha Saadani. Picha 5. Ingawa imefifia katika maelezo ya tangazo la SGR inaonesha kuwa mpaka wa kaskazini mashiriki uliwekwa kwa msitari wa mawe ya bikoni.

Mchoro wa 5: Kifungu cha awali (1974) cha Hifadhi ya Saadani iliyoanzishwa na jamii. Chanzo: Ofisi ya Uchapishaji wa Serikali, Dar es Salaam. Online: https://www.tnrf.org/sw/node/5574

Tangu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Saadani mwaka 2005, mamlaka ya Hifadhi wamechukua hatua kuwaondoa wanakijiji wa Saadani waliokuwa wakiish kwenye maeneo mwawili ya yenye ufukwe kati ya matatu, Uvinje and Porokanya. Viongozi wa kijiji wamejitahidi kupinga tangu mwanzo kabla ya kuwekwa rasmi kwa Hifadhi, kuwa ardhi yao haikuwahi kuwa sehemu ya hifadhi (The Independent Daily Newspaper 2003) na, baadae, wamekuwa wakieleza kuwa wangepinga kuondoshwa katika maeneo yao waliyoyarithi, (Mawio NewsPaper 2013). Mchakato wa kuanzishwa kwa Hifadhi na mpangilio wake, unasaidia kuelezea sababu za migogoro kati ya hifadhi na jamii katika eneo ambalo mwanzo lilitambulika kwa uhifadhi shirikishi uifanikiwa.

Ufanyaji maamuzi ya uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya saadani

Mafaniko ya uhifadhi shirikishi na kuendelea kwa jamii katika uhifadhi wa bayoanuai kwenye SGR kulipelekea baadae kuanzishwa kwa SNP. Mwanzo, pendekezo lilitolewa kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) miaka ya 1990 kuanzisha hifadhi ya kwanza ya Pwani nchini na kufanya ipate mwitikio mzuri mwanzoni mwa kuweka mipango ya hifadhi. Mahojiano na Afisa wa TANAPA aliyehusika katika uanzishwaji wake, Domician Njau, pamoja na taarifa za TANAPA na kumbukumbu za uanzishwaji wa Hifadhi, zinaonesha ushiriki wa jamii katika kuweka mipango ya Hifadhi, kama njia ya msingi ya kupata muafaka na wawakilishi wa vijiji katika mchakato wa uanzishwaji wa Hifadhi (Bagamoyo District Board 2001, 2002; Tanzania National Parks Authority 2002, 2009).

Kwenye taarifa zote za TANAPA, ushiriki wa jamii unaelezwa kama njia kuu iliyotumika kuanzisha Hifadhi (Tanzania National Parks Authority 2002, 2009). TANAPA waliendesha semina kadhaa na vikao vya wadau katika ngazi za wilaya, ambapo wawakilishi wa vijiji walialikwa kujadili uwezekano wa kuanzishwa Hifadhi (Bagamoyo District Board 2002; Tanzania National Parks Authority 2002). Matukio haya yamerekodiwa wilayani, inaelezwa idadi ya mikutano na mada zilizojadiliwa na wilaya na wajumbe wa vijiji. Hata hivyo hakuna rekodi iliyopitiwa kwenye utafiti huu pamoja na eneo la kijiografia la hifadhi, mipaka, na kiasi na maeneo ya ardhi ya vijiji ambayo ingeingizwa katika eneo la hifadhi. Kama ilivyoelezwa, vikao vya kuomba ridhaa ya viongozi wa vijiji vilikuwa ni kulingana na maelezo ya TANAPA juu ya umuhimu wa kiikolojia wa kuanzisha hifadhi, isipokuwa ngazi moja ya wilaya, TANAPA iliwasilisha ramani moja ya SGR iliyotengenezwa na TANAPA. Katika mkutano huo ramani ya tanapa ya SGR ilipewa kwa viongozi wa wilaya ya Bagamoyo na washiriki wa kikao wakapitisha kuanzishwa kwa SNP (Tanzania National Parks Authority 2002).

Picha na.6 ni ramani ya usimamizi wa zamani na umiliki, na ardhi ya sasa ya eneo la SNP, matumizi ya ardhi, mipaka ya zamani ya vijiji na maeneo muhimu ya vijiji vinavyopakana na Hifadhi. Muhimu zaidi miongoni mwa matumizi mbalimbali ya ardhi ni hifadhi za vijiji na maeneo ya akiba na maeneo yenye usimamizi maalum ambayo yanazunguka hifadhi ambayo yalikuwepo kabla ya kuanza kwa hifadhi. Eneo la kaskazini la hifadhi kwa kiasi kikubwa ni la Ranchi ya Mkwaja na kiasi kidogo cha yaliyokuwa maeneo ya uvuvi na ardhi ya vijiji. Kadhalika, eneo la kusini la hifadhi limegawanyika sehemu mbili; maeneo ya zamani ya vijiji na maeneo ambayo awali yalisimamiwa na wilaya au mashirika ya kitaifa. Maeneo ambayo yalikuwa chini ya serikali ni pamoja na Hifadhi ya Msitu wa Zaraninge, (zamani ulisimamiwa na wialaya ya Bagamoyo), kipande cha eneo la RAZABA (zamani lilimilikiwa na Serekali ya Zanzibar). Picha na. 6 pia inaonesha ramani ya TANAPA ya SGR ambyo ipo Idara ya Wanyamapori.  Ramani hii ya SGR mipaka yake ndiyo iliyotumiwa kuwaelezea waliofanya maamuzi wilayani juu ya uanzishwaji wa SNP (Tanzania National Parks Authority 2002).

Picha ya 6: Usimamizi wa zamani na umiliki wa ardhi unaojumuisha SNP na umuhimu wa ardhi za bustani na majina muhimu ya matumizi ya ardhi karibu na SNP. (Vyanzo: Mpango wa usimamizi wa Hifadhi ya Saadani 2010-2020, Ofisi ya Takwimu ya Takwimu ya 2002, Ripoti ya Ufundi na wengine waliotajwa)

Uchambuzi wa Kiramani wa Pori la akiba la Saadani na Hifadhi ya Taifa ya Saadani

Uchambuzi wa Kiramani ulitumika kuweka pamoja taarifa zote kwenye SGR na mipaka mengine ambayo ililetwa kwenye SNP na kuangalia utofauti wa mipaka inayohusiana na SGR na kijiji cha Saadani. Hii inaoneshwa kwenye picha na. 7, ambayo kushoto inaonesha ramani ya TANAPA ya SGR na SNP na eneo la zamani la kijiji, upande wa kulia, ni ramani mbili zilizowekwa pamoja na kukuzwa za SGR, moja ni ile inayotoka TANAPA (iliyotengenezwa kati ya 1999 na 2001 kama inavyooneshwa kushoto) na nyingine kutoka kwenye ripoti ya utafiti wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (ya 1996-1997, Picha na. 4, juu). Katika ramani hiyo kumeongezewa eneo la kitongoji cha Saadani na mipaka ya awali ya SGR wenye mawe ya bikoni yalizogunguliwa na wanakijiji na waandishi (wa makala hii) kipindi cha 2012 – 2014 ambacho mradi huu ulifanyika. Kama inavyoonekana, ramani mbili zilizowekwa pamoja za SGR zinaonesha eneo la kijiji cha Saadani limeingizwa kama sehemu ya SNP na eneo la ardhi lililoachiwa kijiji cha Saadani.

Si ramani ya zamani SGR wala ramani ya utafiti wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ya 1997 inayoyoonesha kuwa mipaka ya mashariki ya hifadhi ilifika baharini. Kwa kutafsiri hili, Idara ya Wanyamapori haikuwahi kuingiza eneo la pwani la kitongoji cha Uvinje na Porokanya kama sehemu ya SGR. Ramani ya TANAPA ya SGR inaonesha mipaka tofauti kabisa ya hifadhi upande wa mashariki, mpaka ambao unaonesha kuwa maeneo yote ya Uvinje, Porokanya na baadhi ya sehemu ya katikati ya kijiji cha Saadani zilikuwa sehemu ya SGR. Hakuna kumbukumbu inayoonesha kuongezwa kwa eneo la SGR wakati hadi kufikia maneo hayo. Wala hatukupata taarifa yoyote inayoashiria viongozi wa wilaya kufahamu mabadiliko yaliyofanya kwenye ramani ya awali ya SGR ilipotolewa ramani ya TANAPA ya SGR wilayani wakati wa kupata ridhaa ya Hifadhi.

Kutokana na kumbukumbu za uanzishwaji wa Hifadhi, TANAPA wamekuwa wakiendelea kudai kuwa eneo la Uvinje muda wote limekuwa ndani ya eneo la hifadhi. (Tanzania National Parks Authority 2002, 2014a).  Ramani mpya ya TANAPA ya SGR imetengenezwa wakati wa jitihada za mamlaka ya Hifadhi kubadilisha makubaliano ya awali yaliyoafikiwa na wazee wa Saadani (inaoneshwa kwenye tanagzo la SGR Picha na.5) na kudai kuwa ardhi hiyo imekuwa muda wote ndani ya eneo la SGR na sasa linamilikiwa na Hifadhi (Tanzania National Parks Authority 2014b).

Picha na. 8, inaonesha tafsiri ya TANAPA ya tangazo la Hifadhi la SGR la mwaka 1974, mchakato wa TANAPA wa kuhalalisha utofauti wa mipaka ya SGR. Kwa suala la ardhi ya kitongoji cha Uvinje, maelezo ya mipaka ya ramani ya 1974 yanaongezea msitari unaosema “hadi mto unapoingilia bahari” na “kutoka maingilio ya mto Mligaji …(kando ya Pwani) na kuondoa mstari unaosema “..halafu kuelekea kusini kufuata mstari wa mawe ya bikoni…”    (angalia mstari wanne wa tangazo halisi la SGR la mwaka 1974, picha na. 5 juu). Kwenye maelezo kuhusu eneo la Porokanya, TANAPA wameongeza mstari unaosema “hadi mto Wami unapoingilia baharini” – Mstari wa 9).

Kwa maumbile ya maeneo ya Saadani na hali ya mvua, wakati wa mvua, mifereji inaweza kuongezeka hata kwa kilometa 3 kwenye maingilio ya mito. Hali hii inaweza kutoa sababu ya kwa nini tangazo rasmi linalezea kuwa mpaka wa mashariki wa SGR unaendelea hadi maingilio ya mto Mligaji na/au Mto Wami. Kwenye tangazo rasmi la SGR la 1974 (Picha na. 5) imeandikwa “mstari wenye mawe ya bikoni” uliwekwa ili kuwa mpaka kati ya Uvinje na upande wa kusini. Tafsiri ya TANAPA ya tangazo rasmi la SGR limekiachia kijiji cha Saadani kilometa 12 za mraba kama sehemu iliyobaki ya eneo la kijiji chao ambapo baadhi ya sehemu yake hupata mafuriko ya msimu na sehemu nyingine kutumika kwa kutengeneza chumvi.

Picha na 7: Kushoto – Ramani za TANAPA za SGR na SNP na kulia ni ramani hizo mbili zimewekwa pamojana kukuzwa. (Chanzo: Mpango wa Usimamizi – Hifadhi ya Taifa ya Saaddani 2010 – 2010, Ripoti ya Utafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1997, Taarifa za ardhi za msingi)

Hakuna hati rasmi zinazohusiana na uanzishwaji wa Hifadhi zinazoonesha namna ardhi ya Saadani ilivyoingizwa kwenye eneo la hifadhi. Wala hatukuweza kupata vithibitisho vyovyote kuwa TANAPA walieleza hili lingetokea, mfano kwenye mkutano rasmi wilayani Bagamoyo. Kinyume chake, hati zinazohusiana na uanzishwaji wa hifadhi kwenye eneo karibu na Saadani inaeleza wazi uongozi wa hifadhi waliahidi kurudisha kijijini eneo la kilometa 1.5 kama “buffer zone” kutoka kwenye eneo la SGR (Kikao cha Bodi, Bagamoyo 2002: Mamlaka ya Hifadhi Tanzania 2002). Zaidi, mpaka wa zamani wa mashariki haukusogezwa magharibi ili kutekeleza ahadi hii, badala yake umesogezwa hadi Pwani kuingiza karibu kilometa za mraba 50 ya eneo ambalo awali viongozi wa kijiji waliliacha kwa ajili ya makazi yao, na kuwaachia kilometa 12 pekee za mraba kama ndio eneo lao lote. Ramani ya SGR iliyotumiwa na TANAPA (Tazama picha na. 7) na maelezo yake ya mipaka ya SGR (Picha na. 8) inaonesha mchakato uliofanywa na TANAPA kupora haki ya umiliki ya kijiji

Picha na. 8: Hati inayoonesha tafsiri ya TANAPA ya Tangazo rasmi la SGR la 1974 – lilioneshwa kwenye picha na. 5. Chanzo: 2014 Barua kutoka TANAPA (Ref No. LAG/SA/1) kwenda kwa wana sharia wa Environmental Action Team (LEAT)

Hifadhi ya migogoro kwenye Uhifadhi – Mandhari rafiki ya kijamii

Mikakati ya Hifadhi ambayo imekuwa ikitekelezwa tangu mwishoni mwa miaka ya 1990 na kuitwa jina la “shirikishi” haijaweza kuzuia SNP iliyoanzishwa rasmi 2005, isikumbwe na migogoro tangu kuanza kwake, ikiwa ni pamoja na migogoro ya ardhi na mipaka kwenye maeneo yake. Imekuwa ni vigumu kuelelea uhifadhi wa bayoanuai na takwimu za Hifadhi zinaonesha kuongezeka mara saba zaidi kwa ujangili tangu kuanza kwa Hifadhi. Ambapo 2005 kulikuwa na makosa 32 yaliyoripotiwa, na mwaka 2011 idadi ya makosa imekuwa ni 224 (Hifadhi ya Taifa ya Saadani 2013). Migogoro ya ardhi ya Hifadhi na mipaka imeibuka kote vijijini na wilayani, na inakuwa ni kwa sababu ya eneo la zamani la hifadhi (SGR na Ranchi ya Mkwaja) na maeneo mapya ya vijiji yaliyochukuliwa (Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo 2005: Kijiji cha Matipwili 2011). Zaidi, imekuwa ni kesi maarufu ya kijiji cha Saadani, ambacho umuhimu wake ulitambuliwa wakati wa kuwekwa majina ya SGR na Hifadhi, kurudiwa kupangiliwa kumesaabisha madhara makubwa ya ushiriki wa jamii kwenye uhifadhi wa mazingira na haki za kumiliki ardhi.

Kiuhalisia, vingozi wa zamani wa kijiji cha Saadani waliwezesha kuundwa kwa SGR kwa kutoa karibu ya 40% ya eneo lao (kadirio la kilometa za mraba 300), na baadae kukubali kutoa 45% (kadirio la kilometa za mraba 128) ya eneo la nchi kavu kwa ajili ya kuanzishwa SNP, na kujibakishia kiasi cha 15% ya eneo la awali (kadirio la kilometa za mraba 50). Mchango huu wa jamii kwa Maeneo yanayohifadhiwa (PA) ulitiwa moyo na mashirika ya kimatafa (Baldus, Roettcher and Broska 2001; Treydte 2004) na kupewa nguvu na mashirika ya kimataifa ya uhifadhi na mengineyo, ikiwa ni pamoja na GTZ, WWF na Fondo Per la Terra (Bagamoyo District Board 2001). Jumla ya mchango wa ardhi ya Saadani kwenye uhifadhi unaosimamiwa na serekali si chini ya 80% ya eneo lake lote, na ilifanyika licha ya kuwa Saadani na vijiji vingine vya pembezoni vilikuwa na maneo ya hifadhi yanayofikia angalao 20% ya eneo la Hifadhi. Vilevile, hadi mwaka 2017 wanakijiji walikuwa wanamiliki kilometa za mraba 11.8 tu kati ya 50 walizobakishiwa kwa makazi yao.

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, wakazi wa vitongoji vya Uvinje na Porokanya wamekuwa wakiitwa wavamizi katika maeneo yao ya urithi na wamekuwa wakikabiliwa na vitisho vya mara kwa mara vya kuwondoa kutoka kwa mamlaka ya Hifadhi (Mwinyamane 2003; Tanzania National Parks Authority 2014b; Uvinje Subvillage 2002, 2003). Mijadala iliyofanyika kwa makundi na kutembelea maeneo ya utafiti pamoja na wajumbe wa halmashauri ya kijiji, serikali ya kijiji, wengi wao wakiwa ni kizazi cha pili au cha tatu cha waliokuwa vinara wa uhifadhi, kunaonesha kuwa viongozi wa kijiji wanaona mamlaka ya Hifadhi wanatenda kama wao wenyewe ni serikali. Pia tumegungua kuwa kuna uchache wa ufahamu wa mipaka ya sasa ya Hifadhi inayokizunguka kijiji, uelewa mdogo wa makubaliano ya mipaka wakati wa SGR na hivyo hakuna upashwaji taarifa juu ya mtazamo wa kisheria wa haki ya ardhi yao kwa vitongoji vya Uvinje na Porokanya.

 

Kwa zaidi ya muongo mmoja, matamko ya TANAPA yanawataja wakazi wa vijiji vya pembezoni mwa pwani kuwa ni wavamizi, “…Kitongoji (cha Uvinje) kipo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria. Kosa lilifanywa kuruhusu watu kukaa pale na idadi yao ikaongezeka baada ya muda” (Tanzania National Parks Authority 2002: 4); “Kitongoji (cha Uvinje) kipo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria. Lilikuwa ni kosa kuruhusu watu kukaa na kuongezeka idadi kwenye eneo hilo…” (Bagamoyo District Board 2002: 4); “Kitongoji cha Uvinje kimekuwa ndani ya mipaka ya SGR na watu wa eneo hili wamekuwa wakiishi ndani ya SGR hata wakati wa kupandisha cheo kuwa Hifadhi…ni dhahiri kuwa wakazi wa Uvinje wapo ndani ya eneo la hifadhi na wanaishi hapo kimakosa. Jitihada za kuwaondosha hawa watu kutoka hifadhini zinaendelea.” (Tanzania National Parks Authority 2014b: 2). Kuendelea kurudiwa kwa kauli hizi kumesababisha baahi ya viongozi wa vijiji kukata tamaa ya kupigania haki ya eneo lao na kupoteza nafasi ya kupata suluhisho mapema kwa mgogoro wa ardhi ambapo kuna vielelezo vinavyoonesha mipaka asili ya SGR.

Wakazi wa Uvinje ambao waliwezesha na kushiriki katika usimamizi wa uhifadhi kwa ngazi tofauti za kiofisi na ulinzi, wamekuwa wakionyesha ari ya kusaidia uhifadhi kupitia kukataa vitendo vya ujangili na walifikia maamuzi kwa pamoja kuacha kazi ya kuchoma chumvi. Hii ilikuwa ni kwa sababu ya madhara yake kwa uhifadhi ingawa ilikuwa ndio shughuli yao kuu ya kuingiza kipato (Mwinyamane 2003). Hata hivo TANAPA walijaribu kukodisha haya maeneo kwa wawekezaji wa kimataifa ili kujengwa hoteli za kitalii za kutumia mahema (Tanzania National Parks Authority 2011). Wito huu wa kutafuta wawekezaji haukuzingatia kuwa wakazi wa Uvinje walikuwa wakikaribia kumalizia hoteli ya kijamii waliyokuwa wakiijenga tangu mara baada ya kuanzishwa kwa hifadhi mwaka 2006. Wao walikuwa ndio wabia na wangekuwa wasimamizi wakuu wa hotel hiyo (The Republic of Tanzania and Ministry of Rights and Human Settlements Development 2009).

Njia za Kimataifa kulisemea suala hili zilifanyika kupitia:

 

  1. Barua sita za rufaa zilitumwa kwa Rais wa sasa na aliyetangulia wa Tanzania, kutoka shirika la Global Consortium of Indigenous and Local Communities’ Conserved Territories and Areas,
  2.  Barua ziliandikwa kwa Umoja wa nchi za Afrika na kitengo maalumu cha haki za watu asilia walio wachache cha Umoja wa Mataifa
  3. Misaada ya kisheria inayoendelea kutoka mashirika ya kimataifa.

Jitihada hizi zilipendekeza kuangaliwa upya suala la haki ya ardhi ya wakazi wa Saadani na kushirikishwa kwao kwenye uhifadhi. Mambo haya ambayo si sahihi yameoneshwa pia katika tafiti zingine tatu (Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora 2017; Kituo cha Msaada wa Kisheria 2017; Ngorisa, Tenende na Msuya 2014). Mojawapo ikiwa ni utafiti ulifanywa na waangalizi wa Tanzania ambao ulitoa hitimisho kuwa kitendo cha TANAPA kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Saadani “kilienda kinyume na matakwa ya sheria” (Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora 2017: 1). Jitihada zote hizi zimeleta mafanikio kidogo katika kutatua tatizo ambalo linahitaji nia ya kisiasa.

Mjadala

Uvamizi wa namna mbalimbali wa watendaji wa serekali kwa miaka kwenye eneo la Saadani umekuwa na madhara ya moja kwa moja kwa taasisi na mipangilio ya uhifadhi; hata hivyo matokeo yanaonesha kuwa ni uanzishwaji wa SNP uliokuwa na madhara zaidi kwenye jitihada za uhifadhi. Eneo hili, ambalo lina utajiri wa bayoanuai limekuwa na historia ya uzalendo wa kijamii. Hata hivyo uanzishwaji wa SNP ulikuwa ni nukta ya kubadilisha hali hiyo. Matokeo juu ya ushiriki wa jamii, au kukosekana kwake, katika kuweka upya mipaka au kupitia makubaliano ya awali, pamoja na kutokuwepo kwa upashwaji taarifa kipindi cha kutengeneza mipango na kufanya maamuzi, kunaonesha kuna utofauti mkubwa kati ya kauli ya serekali juu ya ushirikishwaji wa jamii katika kupangilia masuala ya uhifadhi na uhalisia ulivyo katika ushiriki wa kupanga uhifadhi ambao ungewawezesha jamii kucheza nafasi yao katika kuhifadhi mazingira.  Wanavijiji na idara za ngazi za wilaya, kama ilivyoelezwa juu, wanapata taarifa chache na hivyo kutoweza kujua taarifa ipi si sahihi. Ushiriki usiokidhi wa viongozi wa kijiji wakati wa uanzishwaji wa Hifadhi umeipa mwanya TANAPA kubadili maafikiano na mipaka ya awali ya Jamii na idara husika.

Madhara yaliyosababishwa na TANAPA yamekuwa na sura nyingi. Wanakijiji wa saadani walithibitisha kupenda uhifadhi wa mazingira, kama ilvyyooneshwa kuwa zaidi ya kumuomba Mkuu wa Idara ya Wanyamapri kuwasaidia, walisaidia kutekezeka kwa kutoa sehemu ya ardhi ya kijiji chao kuanzishwa SGR. Vitendo vya TANAPA vimevuruga hatua zilizochukuliwa na jamii hii katika kuhifadhi mandhari ya mazingira yao na kuwafanya wawe hawana ardhi na kushindwa kujimudu kwenye mchakato.  Takwimu za hivi karibuni za ujangili na kuongezeka kwa manung’uniko ya jamii kunaashiria kuwa kuanzishwa kwa SNP si tu kumekuwa na madhara kwa wanakijiji bali pia kumeharibu mafanikio ya uhifadhi yaliyopatikana miongo ya nyuma.

Jitihada za TANAPA kupata udhibiti wa utajiri wote wa kimazingira na maeneo muhimu kitamaduni na kitalii, umepewa nguvu na mashirika ya kimataifa ya uhifadhi. Hili pia linaelezea namna gani mikakati ya serikali ya utawala na usimamizi wa maeneo yanayohifadhiwa inaweza kuharibu nafasi ya kufanya uhifadhi kuwa jitihada za kugusa ngazi tofauti zinazokubaliwa na mashirika ya kitaifa, kimataifa na jamii ambazo maeneo yao yamekusudiwa kwa uhifadhi. Nafasi ya wanakijiji wa Saadani na hatua ya kuanzisha hoteli ya kijamii inayojali utunzaji wa mazingira inaleta ugumu wa kuhalalisha kunyang’anywa ardhi yao ya urithi na makazi na wanakijiji hawa walionesha kuwa hawana madhara kwenye uhifadhi zadi ya kuwa wangesaidia jitihada hizo. Kinachoonesha kuwa kuna nia zaidi ya kutengeneza faida kuliko ya kufanikisha uhifadhi, ni wito wa mamlaka kwa wawekeaji wa utalii wa kimataifa kukodisha ardhi, wito ambao ungewasaidia kuongeza faida, licha ya jitihada za jamii za kushiriki katika utalii endelevu tangu 2006, kutekeleza hilo kwa idhini ya mkono mwingine wa serekali.

Ingawa kuna utofauti wa wazi kati ya modeli ya sasa ya sheria kali za uhifadhi unaosimamiwa na serekali, ambao unawatenga watu kutoka kwenye mazigira yanayohifadhiwa, na ile modeli ya kijadi ambayo watu wanachukuliwa kama sehemu ya mazinngira, hizi tofauti sizo zinazoleta migogoro eneo la Saadani. Hakika, kuna tofauti kubwa kati ya uzalendo wa kimazingira wa wanajamii na uhifadhi unaosimamiwa na serikali, lakini kinacholeta migogoro ni usimamizi wa serikali unaoleta maswali kwa kile knachoonekana kuwa ni usmamizi shirikishi wa mazingira. Kama matokeo ya utafiti yanavyoonesha, mipango ya TANAPA ya uhifadhi na usimamizi si tu imesababisha wanakijiji wanaojali uhifadhi kupoteza ardhi yao lakini pia ni kikwazo katika kufikia Malengo ya Uhifadhi ya Aichi A, D na E: kuongelea sababu halisi za upotevu wa bayoanuai, Kuhakikisha mafanikio ya wote wanaoshiriki katika kuweka mipango ya uhifadhi na kuhifadhi kwa njia shirikishi.

Idadi kubwa ya tafiti inaonesha kuwa maeneo yenye utajiri wa kimazingira ambayo yalikuwa chini ya usimamizi wa jamii yamechukuliwa na sasa yanasimamiwa na Taifa na watendaji wa kimataifa. Kwa Tanzania, huu umekuwa ni msukumo wa kuongeza ukubwa wa Maeneo yanayohifadhiwa (PA) (Brockington and Igoe 2006; Benjaminsen and Bryceson 2012) na duniani pia (Brockington and Igoe 2006; Dowie 2011; Juffe-Bignoli et al. 2014). Kama ilivyo, kubadilishwa mgawanyo wa ardhi unaofanywa wakati wa kuanzisha maeneo ya hifadhi, kumeathiri mifumo ya usimamizi na umiliki wa ardhi na maliasili ya jamii (Benjaminsen et al. 2013; Brockington, Duffy, and Igoe 2008; Goldman 2003; Hoole and Berkes 2010). Hata hivyo, kesi ya Saadani isiwe tu ni mfano mwingine wa namna ambavyo usimamizi wa hifadhi wa serikali umekuwa zana ya kuvuruga maisha ya wanajamii (Brockington 1999; Clements et al. 2014), au namna uhifadhi wa kutumia mabavu unavyoendelea kusababisha watu kupoteza haki ya kumiliki ardhi kwa kisingizio cha kutekeleza manufaa ya umma kutoka kwenye mazingira yanayohifadhiwa. Mchango mkubwa wa matokeo ya utafiti huu ni katika kuonesha mchakato unaofuatwa na uhifadhi unaosimamiwa na serekali- licha ya malengo ya kimataifa – na namna gani haulengi katika kuleta ushiriki wa jamii na si kila mara unafanywa kwa malengo ya kuhifadhi mazingira

Matokeo ya utafiti huu yanaongezea juu ya wasiwasi unaozidi kukua wa misingi na mikakati ya uhifadhi unaosimamiwa na serekali kutokujali utofauti ulipo duniani wa tamaduni na umiliki, na namna wanavyofananisha vitendo vinavyosababisha upotevu wa bayoanuai kote duniani (Agrawal and Redford 2009; Chapin 2004; Colchester 1994; Dowie 2011; Neumann 1998).

 

Wanaelekezea vidole mambo yasiyofanana na kuhamisha mijadala inayohusiana na uhifadhi isijadili utengwaji wa watu na kupotezewa haki za umiliki wa ardhi. Wanalazimishia tathmini ya malengo ya uhifadhi ya dunia ambayo yanaelezea maendeleo ya uhifadhi kama misingi ya uwakilishi na ukubwa wa maeneo yanayohifadhiwa, ambayo taarifa zake hutolewa na takwimu za kiikolojia na unatilia mkazo katika jitihada za usimamizi (yaani nini kifanyike) kuliko mtazamo wa kiusimamizi (yaani, nani anafanya maamuzi na namna gani anafanya hayo maamuzi)

Usimamizi wa ufanisi na haki ni ufunguo wa kuleta mafanikio ya kijamii ya maisha mazuri na usawa na malengo ya uhifadhi wa mazingira. Kwa msingi huu suala la Saadani linaonesha wasiwasi juu ya mambo hayo mawili ya msingi. Haya ndio mahitaji ya kuelezea tena nini kinachoomaanishwa na kauli ya “uhifadhi shirikishi” katika muondo wa sasa wa uhifadhi, na haja ya kubadilisha nafasi ya serikali kuwa ya ufikishaji na kiunganishi kati ya jitihada zajamii na vyanzo vya kimataifa vya uhifadhi kuliko kuwa wapangaji na watekelezaji wakuu (na wafanyaji wakuu wa maamuzi ya kiutawala) katika mipango ya uhifadhi na mijadala.

Hitimisho

Makala hii imewasilisha tathmini ya mikakati ya uhifadhi unaosimamiwa na serekali, ufanyaji maamuzi na usimamizi, na mgawanyo wa ardhi katika eneo la Saadani limekuwa na madhara kwa jamii wanaoshiriki uhifadhi na kwa jitihada za kuleta uzalendo wa kimazingira. Ingawa haki na ushiriki wa jamii katika uhifadhi zimeingizwa katika tamko la sasa la kimazingra la Tanzania na dunia, utafiti huu unaongezea kesi zinazoelezea haki hizi hazieleweki wala kutekelezwa kwenye ngazi za utendaji.

Malengo ya mamlaka za serekali juu ya usimamizi wa ardhi, mtazamo wao wa dhahiri wa mipaka, na namna ya ushiriki wa pamoja ambao malengo yake yamewekwa na taasisi za uhifadhi ndizo nguzo za uhifadhi unaosimamiwa na serekali. Kwa mtazamo huu, mgawanyo mpya wa ardhi ndio nyenzo inazoweza kutimiza mikakati ya uhifadhi ya usawa na yanaweza kufanikisha usawa na ufanisi wa uhifadhi. Mgawanyo mpya wa ardhi utabadilisha hali ya ushirikiano miongoni mwa vitengo vya kijamii na vile vya kiserekali. Inaathiri usimamiaji na kiwango cha mamlaka yanayoshikiliwa na watendaji tofauti, vitengo vya jamii vya usimamizi wa ardhi na utekelezaji wa atendaji wa jamii, ambao ndio waliowezesha kufanikisha uendelevu wa kiikolojia na usimamizi wa ardhi. Saadani, usimamizi wa sekali wa mazingira na mgawanyo wa ardhi, zaidi ya kuufanya utaratibu wa Hifadhi kuwa mgumu kubebeka na jamii wanaojali uhifadhi wa mazingira, matokeo yake yanaleta maswali juu ya nafasi ya inayoshikiliwa na srekali kuwa watendaji wakuu wa kutekeleza maazimio ya uhifadhi.

Kukusanya misaada kwa ajili ya masomo ya Sayansi ya Mazingira na Sayansi ya Jamii inaelezea haja ya kuwa na mikakati kamili ya kuhifadhi mazigira (Mfano., Mora and Sale 2011; O’Riordan and Stoll-Kleemann 2002) na inaelezea kuwa “uwezo wetu wa kujua kipimo cha tunayoyafanya na nini kinahitajika kufanyika kimsingi kutusogeza mbele, matokeo endelevu hayajawahi kufanyiwa tathmini” (O’Riordan 2002: 4). Makubaliano ya sasa ya kimataifa ya uhifadhi kama vile Maafikiano ya Uhifadhi wa Bayoanuai, yapo katika kutekelezwa yakiangalia zaidi ukubwa wa maeneno yanayohifadhiwa (PAs), ambapo yana fursa ya kuelezea ushirkishwaji katika kuweka mipango na kuitambua elimu ya jadi (Convention on Biological Diversity 2010), yanakosa mikakati yenye ufanisi ya kuhakikisha ushirikishwaji wa haki za ardhi za jamii na za kijadi. Vitu vinavyopelekea kupotea kwa bayoanuai kwa sasa – ujangili, matumizi ya rasilimali yasiyo endelevu, uharibifu wa mazingira, n.k- yanazidi nguvu uwezo wa jamii yoyote au serikali. Sasa ni muda wa mikakati ya uhifadhi inayoweka serekali kukinzana na jamii kubadilishwa na taratibu zinazoweka mikakati ya uhifadhi kwenye mikono ya jamii, ufanyaji maamuzi shirikishi na usimamizi wa ngazi tofauti.

References

  1. Images: A. Orozco-Quintero
  2. Video and Satellite Images: Google Earth, Image IBCAO. Data SIO NOAA, US Navy, GAO, GEBCO
  3. Agrawal, A. and K.H. Redford. 2009. Conservation and displacement: an overview. Conservation and Society 7(1): 1.
  4. Alcorn, J.B. 1993. Indigenous peoples and conservation. Conservation Biology 7(2): 424–426.
  5. Aubertin, C. and E. Rodary (eds.). 2011. Protected areas, sustainable land? Farnham: Ashgate.
  6. Bagamoyo District Board 2001. Minutes of the District Board Meeting of the Committee on Proper Land Utilization on 9/11/2001 at Bagamoyo District Commissioner’s Office.
  7. Bagamoyo District Board 2002. Minutes of the District Board Meeting on 31/1/2002 at Mantep Hall, Bagamoyo District. Bagamoyo, Pwani. Tanzania: BDB.
  8. Bagamoyo District Commissioner 2005. Dispute between TANAPA and residents of Miono Division, Mkange location, Saadani, Matipwili-Java, and Mkange villages.
  9. Baldus, R.D., K. Roettcher and D. Broska. 2001. Saadani: an introduction to Tanzania’s Future 13th National Park. In R.D. Baldus and L. Siege (eds.). Tanzania Wildlife Discussion Paper 30. GTZ and Wildlife Division Tanzania.
  10. Barrett, C.B., K. Brandon, C.C. Gibson and H.E. Gjertsen. 2001. Conserving tropical biodiversity amid weak institutions. Bioscience 51(6): 497–502.
  11. Benjaminsen, T.A. and I. Bryceson. 2012. Conservation, green/blue grabbing and accumulation by dispossession in Tanzania. Journal of Peasant Studies 39(2): 335–355.
  12. Benjaminsen, T.A., M.J. Goldman, M.Y. Minwary and F.P. Maganga. 2013. Wildlife management in Tanzania: state control, rent seeking and community resistance. Development and Change 44(5): 1087–1109.
  13. Berkes, F., Folke, C. and Colding, J. 1998. Linking social and ecological systems:  management practices and social mechanisms for building resilience. Cambridge: Cambridge University Press.
  14. Borrini-Feyerabend, G., A. Kothari and G. Oviedo, 2004. Indigenous and local communities and protected areas : towards equity and enhanced conservation: guidance on policy and practice for co-managed protected areas and community conserved areas. Best practice protected area guidelines series 11. Gland, Switzerland ; Cambridge: IUCN–the World Conservation Union.
  15. Borrini-Feyerabend, G., M. Pimbert, M.T. Farvar, A. Kothari and Y. Renard. 2004. Sharing power: learning by doing in co-management of natural resources throughout the world. London: IIED.
  16. Brandon, K., K.H. Redford and S.E. Sanderson (eds.). 1998. Parks in peril: people, politics and protected areas. Washington, D.C.: Island Press.
  17. Brechin, S., G.D. Murray and C.E. Benjamin. 2007. Contested ground in nature protection: current challenges and opportunities in community-based natural resources and protected areas management. In Pretty, J., T. Benton, J. Guivant, D. Lee, D. Orr, M.J. Pfeffer and H. Ward. (eds.) Sage handbook on environment and society. Thousand Oaks: Sage. Pp. 553–577.
  18. Brechin, S., P.R. Wilshusen,  C. Fortwangler and P. West (eds.). 2003. Contested nature: promoting international biodiversity with social justice in the twenty-first century. Albany: State University Press of New York.
  19. Brockington, D. 1999. Conservation, displacement, and livelihoods: the consequences of eviction for pastoralists moved from the Mkomazi Game Reserve, Tanzania. Nomadic Peoples 3(2): 74–96.
  20. Brockington, D. 2002. Fortress conservation: the preservation of the Mkomazi Game Reserve, Tanzania. Oxford: James Currey.
  21. Brockington, D., R. Duffy, and J. Igoe. 2008. Nature unbound: conservation, capitalism and the future of protected areas. London: Earthscan.
  22. Brockington, D. and Igoe, J. 2006. Eviction for conservation : a global overview. Conservation and Society 4(3): 424–470.
  23. Brockington, D., Igoe, J. and K. Schmidt-Soltau. 2006. Conservation, human rights, and poverty reduction. Conservation Biology 20(1): 250–252.
  24. Chape, S., M. Spalding, and M. Jenkins (eds.). 2008. The world’s protected areas: status, values and prospects in the 21st century. Berkeley:  University of California Press.
  25. Chapin, M. 2004. A challenge to conservationists. World Watch Magazine (November/December): 17–31.
  26. Clements, T., S. Suon, D.S. Wilkie and E.J. Milner-Gulland. 2014. Impacts of Protected Areas on local livelihoods in Cambodia. World Development 64: S125–S134.
  27. Colchester, M. 1994. Salvaging nature: Indigenous peoples, protected areas and biodiversity conservation. Discussion Paper 55. Geneva: UNSRID.
  28. Commission on Human Rights and Good Governance 2017. Commission on Human Rights and Good Governance: Inclusion of Uvinje Hamlet as Part of Saadani National Park. Dar Es Salaam, Tanzania.
  29. Convention on Biological Diversity 2010. The Strategic Plan for Biodiversity 2011-2020 and the Aichi Biodiversity Targets. Document UNEP/CBD/COP/DEC/X/2. Nagoya, Japan: Secretariat of the Convention on Biological Diversity.
  30. Craigie, I.D., J.E.M. Baillie, A. Balmford, C. Carbone, B. Collen, R.E. Green and J.M. Hutton. 2010. Large mammal population declines in Africa’s protected areas. Biological Conservation 143(9): 2221–2228.
  31. Department of Wildlife and The Republic of Tanzania 1968. 1968-1976 Saadani Game Reserve monthly reports. Dar Es Salaam, Tanzania.
  32. Dowie, M. 2011. Conservation refugees: the hundred-year conflict between global conservation and native peoples. MIT Press.
  33. Goldman, M.J. 2003. Partitioned nature, privileged knowledge: community-based conservation in Tanzania. Development and Change 34(5): 833–862.
  34. Goldstein, G. 2004. Legal system and wildlife conservation: history and the law’s effect on indigenous people and community conservation in Tanzania. Georgetown International Environmental Law Review 17: 481-
  35. Hoole, A. and F. Berkes. 2010. Breaking down fences: recoupling social-ecological systems for biodiversity conservation in Namibia. Geoforum 41(2): 304–317.
  36. Igoe, J. and Brockington, D. 2007. Neoliberal conservation: a brief introduction. Conservation and Society 5(4): 432–449.
  37. IUCN 2009. World Commission on Protected Areas program. Gland, Switwerland: IUCN
  38. IUCN and UNEP 2013. The World Database on Protected Areas. The World Database on Protected Areas (WDPA). doi: www.protectedplanet.net.
  39. James, A.N., K.J. Gaston and A. Balmford. 1999. Balancing the earth’s accounts. Nature 401(6751): 323–324.
  40. Juffe-Bignoli, D., N.D. Burgess, H. Bingham, E.M.S. Belle, M.G. Lima, M. Deguignet, B. Bertzky, A.N. Milam, J. Martinez-Lopez, E. Lewis, A. Eassom, S. Wicander, J. Geldmann, A. Van Soesbergen, A.P. Arnell,  B. O’Connor, S. Park, Y.N. Shi, F.S. Danks, B. MacSharry and N. Kingston. 2014. Protected planet report 2014: tracking progress towards global targets for protected areas. Cambridge: UNEP-WCMC.
  41. Legal and Human Rights Centre 2017. Uvinje eviction saga: Legal and Human Rights Centre fact-finding mission report on Saadani National Park. Dar Es Salaam, Tanzania: LHRC.
  42. Matipwili Village 2011. Matipwili Village Council Meeting, July 26.
  43. Mawio NewsPaper 2013. Uvinje: the government is seeking to incriminate us. November.
  44. Mora, C. and P.F. Sale. 2011. Ongoing global biodiversity loss and the need to move beyond protected areas: a review of the technical and practical shortcomings of protected areas on land and sea. Marine Ecology Progress Series 434: 251–266.
  45. Mwinyamane, A.S. 1994. History of Saadani Village and Saadani Game Reserve.
  46. Mwinyamane, A.S. 2003. Tanapa organization causes death and anxiety in Uvinje. Dar Es Salaam, Tanzania.
  47. Neumann, R.P. 1998. Imposing wilderness: struggles over livelihood and nature preservation in Africa. Berkeley: University of California Press.
  48. Ngorisa, V., N. Tenende and E. Msuya. 2014. A fact finding mission report on the land dispute between Saadani National Park and Uvinje Villagers. Dar Es Salaam, Tanzania.
  49. O’Riordan, T. 2002. Protecting beyond the protected. In O’Riordan, T. and S. Stoll-Kleemann (eds.) Biodiversity, sustainability and human communities: protecting beyond the protected. Cambridge: Cambridge University Press. Pp. 1–30.
  50. O’Riordan, T. and S. Stoll-Kleemann (eds.). 2002. Biodiversity, sustainability and human communities: protecting beyond the protected. Cambridge: Cambridge University Press.
  51. Packer, C., H. Brink, B.M. Kissui, H. Maliti, H. Kushnir and T. Caro. 2011. Effects of trophy hunting on lion and leopard populations in Tanzania. Conservation Biology 25(1): 142–153.
  52. Peterson, N.D. and C. Isenhour. 2014. Introduction: moving beyond the ‘rational actor’ in environmental governance and conservation. Conservation and Society 12(3): 229-.
  53. Rantala, S. and H. Vihemäki. 2011. Human impacts of displacement from protected areas: lessons from the establishment of the Derema Corridor, north-eastern Tanzania. Paper presented in the 13th Biannual Conference of the International Association for the Study of the Commons, Hyderabad, India, 11–14th January. https://dlc.dlib.indiana.edu/dlc/handle/10535/7104.
  54. Robinson, L.W. and E. Makupa. 2015. Using analysis of governance to unpack community-based conservation: a case study from Tanzania. Environmental Management 56(5): 1214–1227.
  55. Roth, R.J. 2008. “Fixing” the forest: the spatiality of conservation conflict in Thailand. Annals of the Association of American Geographers 98(2): 373–391.
  56. Saadani National Park. 2013. Saadani National Park: 2012-2013. Resource Protection Annual Report.
  57. Secretariat of the Convention on Biological Diversity 2010. Global Biodiversity Outlook 3.
  58. Stevens, S. (ed.). 1997. Conservation through cultural survival: Indigenous peoples and protected areas. Washington D.C.: Island Press.
  59. Tanzania National Parks Authority 2002. Proposal to establish a national park, report to Bagamoyo District Council. January 31.
  60. Tanzania National Parks Authority 2003. Saadani National Park: management zone plan environmental impact assessement. Arusha, Tanzania.
  61. Tanzania National Parks Authority 2005. Community Conservation Services: strategic action plan (2005-2015). Arusha, Tanzania: TANAPA.
  62. Tanzania National Parks Authority 2009. Saadani National Park: General Management Plan 2010-2020. Arusha, Tanzania: TANAPA.
  63. Tanzania National Parks Authority 2011. Tanzania National Parks Authority: invitation for investors. Arusha, Tanzania: TANAPA. Archive copy
  64. Tanzania National Parks Authority 2014a. Saadani National Park: official communication. Dar Es Salaam, Tanzania: TANAPA.
  65. Tanzania National Parks Authority 2014b. Saadani National Park: official communication. Dar es Salaam, Tanzania: TANAPA.
  66. The Independent Daily Newspaper 2003. News: villagers swear to die to protect the village. Dar Es Salaam, Tanzania.
  67. The Republic of Tanzania and Ministry of Rights and Human Settlements Development 2009. Letter of offer of right of occupancy. Bagamoyo, Pwani. Tanzania.
  68. Treydte, A.C. 2004. Ecosystem studies on the former Mkwaja Ranch and the new Saadani National Park between 2001 and 2004. Tanzania Wildlife Discussion Paper 42. GTZ and Tanzania Wildlife.
  69. Underdal, A. 2008. Determining the causal significance of institutions: accomplishments and challenges. In Young, O.R., L.A. King and H. Schroeder (eds). Institutions and environmental change: principal findings, applications, and research frontiers. Cambridge, Massachusetts: MIT Press. Pp. 49–78.
  70. University of Dar Es Salaam and Institute of Resource Assessment. 1997. Environmental evaluation for tourism development in the Saadani Game Reserve. Dar Es Salaam, Tanzania.
  71. Uvinje Subvillage 2002. Letter to the Comission on Human Rights and Good Governance: is this oppression part of human rights and good governance in the country? Bagamoyo, Pwani. Tanzania.
  72. Uvinje Subvillage 2003. Letter to the Bagamoyo District Commissioner: report to vacate the sub-village and pave the way for animals or be forcefully evicted. Bagamoyo, Pwani. Tanzania.
  73. Venter, O., R.A. Fuller, D.B. Segan, J. Carwardine, T.M. Brooks, S.M.H. Butchart, M. Di Marco, T. Iwamura, L. Joseph, D. O’Grady, H.P. Possingham, C. Rondinini, R.J. Smith, M. Venter and J.E.M. Watson. 2014. Targeting global protected area expansion for imperiled biodiversity. PLoS Biology 12(6).
  74. Waldron, A., A.O. Mooers, D.C. Miller, N. Nibbelink, D. Redding and T.S. Kuhn. 2013. Targeting global conservation funding to limit immediate biodiversity declines. Proceedings of the National Academy of Sciences 1–5.
  75. Watson, J.E.M., N. Dudley, D.B. Segan and M. Hockings. 2014. The performance and potential of protected areas. Nature 515(7525): 67–73.
  76. West, P. and S. Brechin (eds.). 1991. Resident peoples and national parks: social dilemmas and strategies in international conservation. Tucson: University of Arizona Press.
  77. West, P., J. Igoe and D. Brockington. 2006. Parks and peoples: the social impact of protected areas. Annual Review of Anthropology 35(1): 251–277.
  78. Wilson, J.A. 2002. Scientific uncertainty, complex systems, and the design of common-pool institutions. In Ostrom, E., T. Dietz, T., N. Dolšak, P.C. Stern, S. Stonich and E.U. Weber (eds). The Drama of the commons. Washington, D.C.: National Academy Press. Pp. 327–360.
  79. World Resources Institute, United Nations Development Program, United Nations Environment Program and The World Bank 2003. World Resources 2002-2004: decisions for the Earth: balance, voice, and power. Washington D.C.: World Resources Institute.
  80. Young, O.R. 1999. Governance in world affairs. Ithaca: Cornell University Press.
  81. Zimmerer, K.S. and K.R. Young (eds.). 1998. Nature’s geography: new lessons for conservation in developing Countries. Madison: University of Wisconsin Press.
  82. Zimmerman, M.A. 1995. Psychological empowerment: issues and illustrations. American Journal of Community Psychology. 23(5): 581–599.